Alhamisi , 20th Apr , 2023

Shirikisho la Soka nchini Tanzania limeweka hadharani Mapato ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Jumapili (April 16).

TFF imetoa taarifa ya mapato ya mchezo huo uliomalizika kwa Young Africans kukubali kuchapwa 2-0, kupitia vyanzo mbalimbali vya Habari vya Shirikisho hilo.

Katika mchezo huo jumla ya mashabiki 53,569 waliingia Uwanjani ambapo VIP A waliingia Watazamaji 340 kwa kiingilio cha sh. 30,000 na kupatikana jumla ya sh. 10,200,000, VIP B waliingia Watazamaji 4,160 kwa kiingilio cha sh. 20,000 ikapatikana jumla ya sh. 83,200,000

Taarifa ya TFF imeeleza: Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliowakutanisha Simba SC na Young Africans uliochezwa Jumapili Aprili 16, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam umeingiza jumla ya sh. 410,645,000.

Katika mchezo huo jumla ya mashabiki 53,569 waliingia ambapo VIP A waliingia Watazamaji 340 kwa kiingilio cha sh. 30,000 na kupatikana jumla ya sh. 10,200,000, VIP B waliingia Watazamaji 4,160 kwa kiingilio cha sh. 20,000 ikapatikana jumla ya sh. 83,200,000.

IP C waliingia watazamaji 2,004 kwa kiingilio cha sh. 15,000 na kupatikana sh. 30,060,000 wakati jukwaa la rangi ya Machungwa waliingia watazamaji 10,372 kwa kiingilio cha sh. 10,000 ikapatikana jumla ya sh. 103,720,000 na jukwaa la mzunguko waliingia Watazamaji 36,693 kwa kiingilio cha sh. 5,000 na kupatikana jumla ya sh. 183,465,000.

Mgawanyo wa mapato

VAT Sh. 62,640.762.71

BMT Sh. 10,440,127.12

Gharama za tiketi Sh. 22,585,475

Uwanja Sh. 47,246,795.28

Gharama za mchezo Sh. 22,048,504.46

TFF Sh. 12,599,145.41

TPLB Sh. 25,198,290.81 FA Mkoa Sh. 18,898,718.11

Timu mwenyeji (Simba SC) Sh. 188,987,181.10