Chama cha Baiskeli nchini Tanzania CHABATA kimeagiza viongozi wa vyama vya mikoa kuwasilisha kalenda zao za michezo kwa mwaka huu,ili kupata kalenda ya pamoja ya matukio ya mashindano ya Baiskeli.
Mwenyekiti wa CHABATA Godfrey Mhagama amesema wanaandaa mkutano wa kupitisha kalenda hiyo kuanzia Januari 15-25, hiyvo vyama vya mikoa viwasilishe kalenda zao kabla ya Januari 12 mwaka huu.
Mhagama amesema kuna mashindano mengi kwa mwaka huu wamepanga kuyaandaa na ametaka makocha na viongozi wa CHABATA mikoani, kuandaa timu zao mapema.

