Jumatano , 27th Sep , 2023

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeipa uwenyeji wa michuano ya AFCON 2027 kwa nchi Tanzania,Kenya na Uganda kupitia kampeni ya PAMOJA BID kwenye Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika leo Jijini Cairo nchini Misri.

Akitangaza matokeo hayo,Rais wa CAF Dr Patrice Motsepe amesema kwamba miongoni mwa vitu vilivyopelekea kushinda kwa uwenyeji huo ni pamoja na utayari wa Marais wa Kenya,Uganda na Tanzania  kuelekea michuano hiyo sambamba na miundombinu na usalama wa watu kwenye nchi hizo.

Hii itakuwa ni fainali za kwanza za Afcon kufanyika ndani ya kanda ya Afrika Mashariki kwa Tanzania,Kenya na Uganda kuandaa pamoja baada ya kuwashinda Misri,Botswana na Senegal huku mara ya mwisho Kenya ilipata nafasi ya kuandaa Afcon 1996 ingawaje shindano likahamishiwa nchini Afrika Kusini.