Alhamisi , 6th Aug , 2015

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesogezwa mbele kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) mpaka Agosti 20 mwaka huu.

Katika taarifa yake, Afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto amesema, awali dirisha la usajili lilikua lifungwe leo na usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti 20 mwaka huu.

Kizuguto amesema, Agosti 21- 28 ni kipindi cha pingamizi ambapo dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kimataifa (FIFA –TMS) litafungwa Septemba 06 huku Ligi Kuu ya Soka Taqnzania Bara ikitarajiw akuanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu.

Kizuguto amesema, vilabu vinatakiwa kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi Novemba 15 mwaka huu.