
Mtoto Neema
Baada ya kumuokoa, raia hao wema walimpeleka katika hospitali ya mkoa wa Katavi ambako hali yake ya afya kwa sasa inaendelea vyema.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa hospitali teule ya Mkoa, muuguzi James Kasabanga, amesema kuwa mtoto huyo wamempokea akiwa katika hali mbaya, ila kwa sasa anaendelea vizuri na amewaomba wasamalia wema kujitokeza kumsaidia mtoto huyo kwani ana uhitaji wa mahitaji muhimu.
Kutokana na jinsi walivyoweza kuokoa uhai wake ,Suzan Tarimo ambaye ni muuguzi katika hospitali hiyo, amesema mtoto huyo wamempa jina la Neema kwa sababu ameokolewa kwa Neema ya Mungu.
Zaidi tazama Video hapo chini