
Aziz Ki and Valentine Nouma
Burkina Faso itakuwa nyumbani Machi 16 2025 kucheza mchezo wake wa 5 wa hatua ya makundi dhidi ya Djibouti kabla ya kusafiri kuwafuata Guinea Bissau tarehe 23 Machi 2025
Ikumbukwe kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwepo katika kikosi kilichocheza mechi za mwanzoni za michuano hiyo akicheza michezo mitatu na kutoa pasi moja ya goli
The Stallions wanashika nafasi ya 3 katika kundi A ikivuna alama 5 katika michezo minne iliyocheza, nyuma ya Guinea Bissau yenye alama 6 na Misri mwenye alama 10 anayeongoza msimamo wa kundi hilo