Jumatatu , 10th Mar , 2025

Mwigizaji Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicolejoyberry leo Machi 10, 2025 amefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa ajili ya kujibu mashtaka ya tuhuma zinazomkabili.

Mwigizaji Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicolejoyberry

Taarifa ya Nicole kukamatwa ilitolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ambapo alieleza wanamshikilia kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufanya biashara ya kuanzisha ma-group na kukusanya pesa kinyume na sheria.

"Matukio haya yametokea ndani na nje ya Dar es Salaam, kwa kuhamasisha baadhi ya watu akianzisha ma-group mbalimbali na kuweka majina hewa kwenye ma-grouup hayo kwamba wanachangia pesa na baada ya muda mfupi basi utapata kiwango kikubwa cha pesa, jambo ambalo baadaye anakuja kutopatikana kwenye simu na kupotea na pesa ambazo watu wamechangia," ilieleza taarifa ya Muliro