Picha ya DJ Choka
Anko Choka ameshea nasi ujumbe huu akiwa kitandani akipatiwa matibabu Hospitali ya Aga Khan.
"Nachopitia mimi kwa sasa ni matokeo ya kuwa mbishi wa kutokwenda Hospitali, hata nikiumwa nilikuwa nasea hii ni Hangover au uchovu wa starehe halafu naendeleza"
"Kuumwa kunaweza kusionekane siku 1 au mwezi lakini ugonjwa unajikusanya tu siku ukija kulipuka ni tukio la mara moja tunakusahau. Nawashauri sana vijana wenzangu kabla ya kupenda bata tuipende miili yetu kwa sababu inatufanya turinge mjini".




