Jumanne , 21st Apr , 2026

Kwenye moja ya mkutano ambao amefanya Msanii mkongwe Akon alizungumza namna ambavyo wasanii wengi wa Marekani wamekuwa wakifeki maisha kujitapa kuwa na magari makali nyumba kali lakini ukweli ni kuwa hawana maisha hayo.

Akiwa katika mkutano huo Akon alifunguka kuwa hiyo ni tofauti sana na Wasanii wa Afrika kwasababu asilimia kubwa ya wasanii hawa kutoka Afrika wanamiliki vitu hivyo na sio vya kukodi kama ambavyo wasanii wa Marekani wanafanya.

Akon alieleza hayo alipokuwa akizungumza kwa ujumla kuhusu Mataifa makubwa Duniani yanavyotumia nguvu kubwa kuaminisha kuwa Afrika ni Bara Maskini sana huku akisema kuwa hiyo ni kinyume na ukweli wa mambo ulivyo