Mimi Mars kama Maua Sama

Alhamisi , 20th Mei , 2021

Wasanii wa Bongo Fleva, Mimi mars na Maua Sama ni mingoni mwa ma-star wanaopendelea kuvaa mitindo mbalimbali ya mavazi na safari hii kwa pamoja wamejikuta wakikutana  katikati ya mtupio wa aina moja.

Pichani kushoto ni msanii Maua Sana na Mimi Mars kulia

Kwenye picha walizo-post instagram kwa nyakati tofauti zimewaonesha kuwa kwenye trend moja ya mavazi, jinsi walivyo pangilia pamba zao pia zimelekeana kwa kiasi kikubwa.

Msanii Maua Sama

Maua ameonekana kuvaa suruali ya ‘jeans’  iliyofifia na kuchanika chanika kwenye magoti huku juu akivalia nguo nyeupe na koti la ‘jeans’, kwa Mimi Mars pia amevalia suruali ya ‘jeans’ ya blue iliyofifia ikiwa imechanwa kiasi juu ya goti la kushoto na shati jeupe.

Msanii Mimi Mars