Jumanne , 4th Jan , 2022

Video zimesambaa mitandaoni zikimuonesha Mchungaji mmoja wa nchini Ghana, akiwavua nguo wanawake na kuwaogesha na kudai kwamba hayo ni maelekezo aliyopewa na Roho Mtakatifu.

Wachungaji wakiogesha na kuwapaka mafuta kondoo wao

Tukio hilo limedaiwa kufanyika siku ya mwaka mpya Jumamosi ya Januari Mosi, 2022, ambapo mmoja akimaliza kuwaogesha mwingine alikuwa akiwapaka mafuta, huku mchungaji anayewaogesha akisisitiza wanawake hao kuwahi.

Katika video hiyo nyuma kuna bango lililoandikwa 'Cross over night'.