
Picha ya mrembo Official Lyyn
Akieleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, Official Lyyn amesema "Mimi naishi maisha ya kawaida kabisa, kwenda hotelini au kula kwenye migahawa ni vitu vya kawaida, wananisema kwamba ninaringa na kujifanya mzuri ila wanasema hivyo kwa sababu hawanijui na hawajawahi kupiga stori na mimi".
"Mtu anakuwa hakujui ndiyo maana anaweza akasema vitu vingi, kama hivyo kuniambia mimi nadanga vitu ambavyo sio vya ukweli, mara nyingi safari zangu ni kwa ajili ya kazi na sio kila kitu unachofanya lazima uwaelezee watu".