Jumanne , 3rd Oct , 2023

Kwenye kuboresha na kuifanya iwe rafiki kwenye matumizi kampuni ya Google, wamepanga kufanya mabadiliko ndani ya ''G-Mail'' na kuipa uwezo wa kutumia ''emoji'' wakati wa matumizi yake.

Picha: WinFuture

 

Maboresho haya huwenda yasiwe mapya kwani yalishawahi kufanywa na ''Microsoft Outlook'' ambayo miaka kadhaa walishafanya maboresho ya namna hii.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutokea ''Google'', zinasema hii itapatikana upande wa kulia wenye vidoti vitatu vile vya ''menu'' ambapo mtumiaji wa G-mail atawezeshwa kuona ''emoji''.

Matumizi ya ''Emoji'' ndani ya ''G-mail'' yanaenda kuwa sehemu ya kurahisisha mawasiliano, kwani yatamuwezesha mtumiaji kuonesha hisia baada ya kupokea ujumbe na kujibu ujumbe kwa njia rahisi zaidi ikiwa kama hakuna uhitaji wa kuandika maneno kwa urefu.