Alhamisi , 20th Jun , 2024

Bibi wa miaka 105 kutokea nchini Marekani, ameteka vichwa mbali mbali vya habari duniani baada ya kuhitimu shahada yake ya umahiri akiwa na umri mkubwa zaidi kutoka chuo kikuu cha Stanford.

 

  

Ginnie Hislop ni mwanamke ambaye alianza safari yake ya kuondoa ujinga kichwani miaka 80 iliyopita, (1940 - )lakini ilishindikana kwa upande wake kuendelea na masomo kwa wakati huo na hii ni baada ya kutokea vita kuu ya pili ya dunia.

Majukumu kwa upande wa Ginnie yalibadilika kutoka kuwa mwanafunzi mpaka kuwa mama wa nyumbani ambaye alihitajika kumsaidia mume wake, Ambaye alikuwa sehemu ya wapiganaji kwenye vita kuu ya pili ya dunia.

Akiwa kama Mama na mlezi wa watoto 2, wajukuu wa 4, na vitukuu 9, haikumzuia yeye kuendelea kuwa sehemu ya bodi ya chuo kikuu cha Stanford, sehemu ambayo alifanikiwa kuandika machapisho kadhaa ambayo yalifanikisha June 16,2024 kutunukiwa shahada ya umahiri.

 

Nb: Shahada ya Umahiri = Master's Degree