
Picha Truphena Ndonga aliyemuua mumewe kwa panga
Truphena Ndonga amesema alijua maisha yake ndio yamefikia ukomo na alidhani angehukumiwa kifungo cha maisha au adhabu ya kunyongwa kutokana na kosa alilolifanya.
Akieleza chanzo cha kumuua mumewe James Oyengo kwa panga Truphena Ndonga amesema hakukusudia kufanya kitendo hicho ila mumewe alikuwa amelewa na kuanzisha ugomvi huku ameshika panga, hivyo akafanikiwa kujiteteta na kumpokonya panga mumewe kisha kumpiga nalo kama njia ya kujikinga.
Aidha ameendelea kusema kwa sasa anaishi kwa kaka yake na anaogopa kurudi nyumbani kwake kwani anajua uchungu wa upande wa ndugu wa mumewe haujaisha pia amepanga kuomba msamaha kwa familia ya mumewe.
Chanzo : Tuko News
Tazama Interview ya Harmorapa akihaha kujibu kuhusu Paula wa Kajala