Jumatano , 5th Jan , 2022

Kwa mara ya kwanza msanii Whozu 'Don Dingoo' amenyoosha maelezo ya chanzo cha kumficha mtoto wake Lola aliyempata na mrembo Cappuccino Tunda.

Picha ya Whozu na mtoto wake Lola

Whozu ameshea video clip ya mtoto wake kwenye page ya Instagram kisha kuandika ujumbe ufuatao.

"Lola mrembo wangu baba yako nilikuficha sana nilitaka ukue vizuri ila walimwengu bahati mbaya wamenizidi nguvu, sisi tumeshaamua kumtegemea Mwenyezi Mungu tu".

"Nikwambie tu mwanangu Instagram ni maisha ya teknolojia utasifiwa, utatukanwa, utaambiwa kila kitu, hilo wala lisikuumize kichwa kwanza sio shida zako mwanangu. Mimi baba yako nipo nyuma yako kwa lolote lile".