Jumamosi , 10th Dec , 2016

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye leo anatarajiwa kutikisa anga la Afrika Mashariki pale atakapoongoza utoaji wa tuzo kubwa za muziki na filamu katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akicharaza gita

Nape Moses Nnauye anaingia kwenye historia ya ulimwengu wa burudani katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa serikali kuongoza na kutoa tuzo katika tuzo ambazo ndiyo zinaanza kutolewa mwaka huu wa 2016.

Huyu ni waziri wa kwanza katika serikali ya awamu ya tano kuongoza wizara hiyo, na katika kipindi cha takriban mwaka mmoja ameonesha ukaribu wa hali ya juu na wasanii, huku akianzisha harakati za kukabiliana na uharamia wa kazi za sanaa kwa kusambaratisha viwanda vidogo ambavyo vimekuwa vikitegeneza na kusambaza kazi feki za wasanii nchini.

Mbali na jitihada hizo, Nape pia ni mdau mkuubwa wa sanaa, kwa maana ya kuwa msanii mwenye uwezo mkubwa wa kucharaza gitaa na kuimba.

Nape anatarajiwa kukabidhi tuzo ya heshima kati ya tuzo 10 zitakazotolewa leo.

Vipengele vingine vinavyowaniwa ni pamoja na Mwanamuziki Bora wa Kiume, Mwanamuziki Bora wa Kike, Wimbo Bora wa Mwaka, Video Bora ya Mwaka, Kundi Bora la Mwaka, Mwanamuziki Bora Chipukizi, Muigizaji Bora wa Kiume, Mwanamuziki Bora wa Kike, pamoja na Filamu Bora ya Mwaka.

Wasanii mbalimbali watawasha moto kwenye stage, ambao ni pamoja na Barnaba Boy, Maurice Kirya kutoka Uganda, rapa mkali Darassa, Shetta, Vanessa Mdee, Wahu kutoka Kenya, Lady JayDee, Ali Kiba aka King Kiba pia Madansa wakali wa shindano la kudansi la Dance100% 2016, washindi Team Makolokocho, Clever Boys pamoja na D.D.I

Wahi tiketi yako sasa kwa utaratibu ufuatao.

 

Tags: