Jumatatu , 17th Mar , 2014

Mwanamuziki wa nchini Nigeria, Tiwa Savage pamoja na Teebillz ambaye ni Meneja wake, wametangaza tarehe ya harusi yao rasmi ni tarehe 26 mwezi April mwaka huu ambapo mpaka sasa shughuli za maandalizi zinakwenda sawa sawa.

Harusi hii imetangazwa kuwa itafanyikia huko Dubai, na kubadilisha mipango ya awali ya kufanyia sherehe hii katika visiwa vya Maldives, ambapo inatarajiwa kuvunja rekodi ya harusi yao ya kimila kwa ufahari, harusi ambayo ilifanyika mwezi Novemba mwaka jana.

Harusi rasmi ya Tiwa pamoja na Teebillz ni kati ya matukio machache ambayo yanangojewa kwa hamu kubwa na wadau pamoja na mashabiki wa muziki nchini Nigeria, katika orodha hii pia ikiwepo harusi ya Paul wa P Square, ambayo itafanyika mwishoni mwa mwezi huu huko nchini Nigeria.