
Timbulo
Hayo yameibuka hivi karibuni baada ya wimbo alioshirikiana na Patoranking kutoka nchini Nigeria uliopewa jina la ‘Koku’ kuvuja na kwamba vionjo vile vinavyopatikana kutoka kwa wasanii ambao wanasimamiwa na uongozi huo wa QS.
Kolabo ilifanikishwa na QS Mhonda, jambo lililozua hisia kuwa huenda QS akawa ama amehusika au amemjumuisha Timbulo katika 'label' yake.
“Siyo label ya muziki Tanzania ambayo inafanya hata muziki ambao unatakiwa Tanzania, hawajui chochote kuhusu muziki hiyo ni label ambayo labda wangekuwa wanafanya vitu vingine kama masuala ya ujenzi na vitu vingine kibao ambavyo mkurugenzi amesomea,” amesema Timbulo
Aidha msanii huyo amesema hawezi kuingia QS kwa kuwa hawezi kukuza kipaji alichonacho maana ameona mifano hai kutoka kwa wasanii wake aliyokuwa nao kushindwa kufikia malengo yao na hatimaye kumkimbia sasa.
Kwa upande mwingine Mhonda amekanusha taarifa za kupata barua ya shukrani kutoka kwa aliyekuwa msanii wake Q-Chief.