Jumatano , 5th Jan , 2022

Msanii wa Ghana Shatta Wale ameendeleza vita yake ya maneno dhidi ya Burnaboy kutoka Nigeria kwa kusema matajiri hawajionyeshi ila masikini ndio wanataka kujionyesha kwa mtu kuwa wana kila kitu.

Kulia ni Shatta Wale kushoto Burnaboy

Shatta Wale ametoa kauli hiyo baada video iliyokuwa ikimuonyesha Burnaboy anatupa pesa kwenye moja ya sehemu za starehe akiwa anakula bata.

"Watu matajiri hawajionyeshi wanaishi kwa kile walichonacho lakini watu masikini wanataka kumuonyesha kila mtu kwamba wana kitu wakati ndani ya moyo wao wanajua hawana, haya niambie sasa nani anakosea hapo, inauma".