Alhamisi , 1st Aug , 2019

Msanii wa kike kutokea nchini Nigeria Seyi Shay, amefunguka kuhusu idadi ya Wanaume ambao amewahi kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Msanii huyo ambaye yupo nchini Tanzania kwa ajili ya Ziara ya kimuziki, amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital wakati alipokuja kwenye kipindi cha 'DADAZ' ya East Africa Television,

"Nimepitia mahusiano na idadi ya Wanaume wengi ambao hawahesabiki na sasa nipo katika mipango ya ndoa. Napenda kuwa kwenye mahusiano na Mtu wa kawaida kwa sababu hawanipi mawazo, wanyenyekevu na watanipa muda wao wa kuwa na Mimi"

Pia msanii huyo amendelea kusema kuwa hapendi mahusiano na watu maarufu kwa sababu wana matatizo sana kama kutokujali na kupenda mashindano.

Baada ya wimbo wa 'Yanje' na Ommy Dimpoz, Msanii huyo amesema anataka kufanya kazi zingine na wasanii wa Afrika Mashariki kama Kaligraph Jones na H-art the band kutokea nchini Kenya, na pia ameshafanya kazi na Vanessa Mdee wimbo unaitwa Skata.