Waziri Mkluu Mizengo Pinda
Hayo yamesema na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda katika hotuba yake kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka 2014/2015
Amesema moja ya hatua zilizochukuliwa ni kufanyika kwa operesheni ya kufuatilia matumizi ya stempu za kodi za Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo zaidi ya stempu milioni moja za bidhaa za filamu zimetolewa.
Jumla ya operesheni nane za kufuatilia filamu zilizoingia sokoni kinyume na taratibu zimefanyika na jumla ya filamu 301 zilibainika kuingia sokoni kinyume na taratibu na wahusika kuchukuliwa hatua.
Mhe. Pinda ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika Nchi nzima na linakuwa endelevu na vilevile, ametoa rai kwa wananchi kununua bidhaa za filamu zenye viwango zinazothibitishwa na uwepo wa stika maalumu.
![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/kigoma all stars.jpg?itok=0eumTa6a)