Alhamisi , 5th Oct , 2023

Biggest Boss Rick Ross amezua gumzo mitandaoni baada ya kusema ametumia Dolla Milioni 100 sawa na Tsh Bilioni 250 na ushee katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.

Picha ya Rick Ross

Akipiga story na #RapLife ya Old Man Ebro #RickRoss anasema ametengeneza mkwanja mwingi kwa muda mrefu ndio maana matumizi yake ya pesa yamekuwa makubwa kama kufanya uwekezaji, biashara na kununua 'Private Jet' yake mpya.

Mashabiki wengi mitandaoni wame-judge Rick Ross kutumia pesa hizo wakisema anadanganya kwa sababu hata utajiri wake wake haufiki pesa alizotumia miezi 6 iliyopita.