Akizungumzia hilo Ray amesema kwamba hawezi kuzuia watu kuongea, lakini ameamua kuachana nao huku akiangalia zaidi mustakabali wa maisha yake.
Ray anafunguka zaidi
“Mimi nawaangalia tu watu wavyosema hovyo. Mara sijui nilikuwa na Tessy, mara Fina (Sarafina) sasa mimi nawaacha wenyewe watajua na kuhukumu wajuavyo, naendelea na mambo yangu,” amesema Ray.
Hata hivyo mama mtoto wake Chuchu Hans amesema kwamba kwa sasa hana muda wa kumfuatilia Ray kwani kama ameshaamua kufanya hivyo hawezi mzuia, na ameshazoea kuumizwa kwenye mahusiano, “unajua kuna wakati mtu unaishiwa hata maneno ya kusema, halafu kingine sina muda tena wa kumfuatilia mtu na kama kaamua hivyo sawa ni kwa faida yake maana wengine tushazoea kuumizwa siku zote”, amema Chuchu Hans.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa wawili hao hawapo pamoja tena, huku Ray akitajwa kuwa kwenye mahusiano mapya na muigizaji wa bongo movie, Sarafina.