Jumatano , 26th Nov , 2014

Rapa Navio ambaye amekuwa nchini Tanzania kwa shughuli zake za kimuziki kwa siku kadhaa sasa, ameiambia eNewz kuwa ndani ya muda huu ameweza kukamilisha kazi kadhaa zikiwepo Kolabo mbili na rapa Izzo Business na msanii Shaa.

msanii wa Hip hop nchini Uganda Navio

Navio amesema kuwa, amefurahia sana muda wake hapa Tanzania, vilevile ushirikiano na wasanii huku akiweka wazi kuwa, Ngoma aliyofanya na msanii Joh Makini itakamilika pindi atakaporudi tena Tanzania siku za karibuni, safari ambayo itasimamiwa na Joh mwenyewe.

Navio amesema kuwa, Wakati wake hapa Tanzania umebanwa kwa sehemu kubwa na ratiba za kazi na hivyo kukosa kabisa nafasi ya kutembelea sehemu za starehe kujionea upande mwingine wa ladha za burudani zinazopatikana Tanzania.