Alhamisi , 30th Jul , 2015

Ari ya wasanii kujiunga na siasa haipo tu Tanzania bali pia hata nchini Uganda, ambapo msanii wa dancehall, Ragga Dee amechukua fomu za chama tawala cha NRM kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya Meya wa Kampala.

msanii wa miondoko ya Dancehall nchini Uganda Ragga Dee

Daniel Kyeyune Kazibwe aka Ragga Dee sasa atachuana na wanachama wengine wa NRM ambao nao wanawania kuteuliwa na chama hicho kupata tiketi ya kupeperusha bendera yake katika nafasi ya umeya.

Ragga Dee amewataka wapiga kura wa Kampala pamoja na wasanii wenzake kumuunga mkono katika nia yake ya kuwania umeya na kuahidi kulibadilisha jiji hilo kuwa kama majiji yaliyoendelea aliyowahi kuyatembelea.