
Mchora Tattoo The Lion Ink kulia akimchora na kumfuta tattoo Kajala
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, The Lion Ink amesema Kajala alimwambia kwamba penzi lake na Harmonize lilienda haraka haraka hivyo mambo mengine alikuwa anashangaa tayari yameshafanyika.
"Ile kauli ya tunatoa uchafu ilitoka kwa Paulah, wakati anarekodi clip mimi na Kajala tulikuwa hatujui kinachoendelea, kwa mimi nilivyoelewa ile tattoo ni kitu ambacho kilikuwa kinamkera sana kwa hiyo kwake hata ile H aliona kama takataka ndiyo maana nikaitoa ile H nikaweka tattoo ya Uaridi" ameeleza The Lion Ink
Mengine zaidi aliyoyazungumza mchora tattoo huyo wakati anafuta tatoo ya H kwa Kajala tazama hapo chini kwenye video.