Alhamisi , 5th Jan , 2023

Msanii wa BongoFleva Barbiemia amesema ipo siku ataziba nafasi ya Vanessa Mdee ambaye kwa sasa yupo busy kulea familia na anaishi nchini Marekani na mchumba wake Rotimi. 

picha ya msanii Barbiemia

"Nitakuja kumreplace Vanessa siku moja kwa sababu sijamuona mtu anafanya kitu kama Vanessa Mdee na haitakuja kutokea na ikitokea haiwezi kuwa kama yeye ila mimi naamini naweza kufanya kitu ikawa zaidi ya Vanessa Mdee". amesema Barbiemia 

Barbiemia amefunguka hilo kupitia show ya Planet Bongo ya East Africa Radio kila siku ya J3 mpaka Ijumaa kuanzia saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.