Jumatano , 19th Dec , 2018

Rais mstaafu wa awamu ya 4 Jakaya Mrisho Kikwete, amesema amefurahishwa na kitendo cha msanii wa Hip Hop Mwana FA, kutambulisha bidhaa ya marashi 'Body Spray' kwa kuwa ni jambo ambalo alimshauri muda.

Kushoto ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kulia ni msanii Mwana FA.

Kikwete ameeleza hayo leo baada ya kutembelewa na Mwana FA nyumbani kwake kwa lengo la kumuonesha bidhaa yake hiyo mpya inayoitwa 'Fyn By Falsafa'.

''Kuna siku nilimsihi Mwana FA na wanamuziki wengine kufanya shughuli nyingine zaidi ya muziki pekee'', ameandika Kikwete kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mstaafu huyo alieyongoza kutoka mwaka 2005 hadi 2015, ameongeza. ''Nimefarijika leo kunitembelea na kutambulisha bidhaa yake mpya ya “body spray”. Hii ni hatua kubwa na nzuri kwa vijana wetu. Tuwaungishe!''.

Mwana FA ni miongoni mwa wasanii mbalimbali ambao wametengeza bidhaa nje ya muziki na sanaa nyingine akiwemo Flaviana Matata ambaye anauza rangi ya kucha iitwayo Lavy pamoja na Jux ambaye anauza nguo kupitia 'brand' yake ya African Boy.