Jumatatu , 7th Nov , 2022

Msanii Nuh Mziwanda ameiambia #PlanetBongo ya East Africa Radio kwamba kuvaa mavazi ya kike yalikuwa lengo ya kuvuta 'Attention' kwa watu kuhusu EP yake mpya ya Wonders.

Picha ya Nuh Mziwanda kwenye mavazi ya kike

"Nilitaka Attetion kwa watu sijafanya kwa ubaya ilikuwa njia moja wapo ya ku-push biashara yangu na kutaka ku-entertain watu. Kitendo cha watu kunitukana ni tayari wanajua kuna EP yangu mpya". amesema Nuh Mziwanda

Show ya Planet Bongo ni kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.