Nikki wa Pili
Amesema hayo akipiga stori na Big Chawa wa Planet Bongo wa East Africa Radio, ambapo amesema kuwa njia rahisi ya kuishi na watoto wa wasumbufu na wasiotaka kusoma ni kutotumia nguvu kama ilivyozoeleka, bali ni msisitizo kwenye mambo ambayo yatawafanya wasome.
"Wazazi na walimu muhimu sana kutambua aina ya wanafunzi walionao, ukienda kila shule lazima kuna wananfunzi wanaojielewa ambao hawashikiwi fimbo na mzazi au mwalimu. Lakini mwanafunzi ambaye hana malengo na hapendi kusoma hata ukikaa naye ukamwambia hakuelewi", amesema Nikki.
"Huyu asiyetaka kusoma ni lazima ajengewe uwezo wa vitu vingine mbalimbali kuhakikisha kuwa anaachana na vile vitu ambavyo vitamzuia kusoma na kumjengea mfereji kuelekea kwenye kusoma, lakini huwezi ukamwambia tu kwa maneno akakuelewa", ameongeza.