Alhamisi , 22nd Mei , 2014

Imepita miaka kumi na moja tangu sekta ya muziki nchini Kenya kumpoteza msanii maarufu E-Sir ambapo licha ya majonzi hayo ya muda mrefu msanii Nameless ameamua kumkumbuka mkali huyo katika siku ya kuzaliwa kwake.

Nameless

Nameless ameelezea kuwa marehemu E-Sir angalikuwapo hai hadi sasa basi hii leo angekuwa anatimiza miaka 33 ya kuzaliwa kwake na kuendeleza muziki wake wa miondoko ya Hip Hop.

Aidha, amewashauri mashabiki, marafiki na familia yake kuendeleza kumkumbuka msanii huyu kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kusaidia kuinua muziki wa Hip Hop.