Alhamisi , 5th Mei , 2022

Msanii wa maigizo, Burton Mwembe maarufu kama Mwijaku, amekutwa na kesi ya kujibu katika shtaka la kusambaza picha za utupu kinyume na sheria linalomkabili.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu,Rhoda Ngimilanga ametangaza uamuzi huo baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wa mashahidi watano na vielelezo vinne.

Mwijaku anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar es salaam.
Msanii huyo anadaiwa kuchapisha picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliounganishwa katika kompyuta.

Mwijaku ataanza kujitetea Mei 10, 2022