Picha ni Msanii Joh Makini, Darassa na Mwana FA
Muziki huu wa Hip Hop mara nyingi mashairi yake huzungumzia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na harakati za ukombozi juu ya jambo fulani na ilikuwa ni agharabu sana kuona au kusikia wimbo wa mapenzi kutoka kwa wanamuziki wa Rap miaka kadhaa nyuma.
Hapa Tanzania kuna baadhi ya nyimbo kali za Hip Hop ambazo zimezungumzia visa mbalimbali kuhusu mapenzi;
Hayakuwa Mapenzi – Mr. II Sugu alizungumzi (Ilikuwa true story) namna ambavyo alitoshwa na mpenzi wake bila hata kujua nini kilisababisha kuvunjika kwa safari yao iliyokuwa imejaa tumaini kubwa juu ya maisha yao ya pamoja kwa muda mrefu hapo baadae.
Chochote Popote (Popote) – Joh makini mwamba wa kaskazini licha ya kuwa hakuwa vizuri kwenye kipato ila aliamini anastahili kuwa na mtoto mkali (mzuri) ambaye anastahili kupata chochote na kumpeleka popote atakapo pendelea kwenda na kumtoa shaka ilimradi tu ampate awe wake.
Kiboko yangu – Hapa binamu alidhihirisha kweli mapenzi yalizaliwa Tanga kama wasemavyo kwani baada ya kusema bado nipo nipo kuna kiboko yake ambaye alimpata mpaka akamsahaulisha yote ya nyuma na kuwa mtumwa wa mapenzi mpaka nusu ya moyo wake akamkabidhi atembee nayo mpenzi wake.
Roho – Fid Q nasema “Mapenzi ni matamu lakini anahofia kuumizwa Moyo, anashindwa kujaribu Roho inamuuma”, “Money makes a man, lakini love ni hustle” moja ya lines kutoka kwenye wimbo huu wa Legend Fid huku King of the best Melody Christian Bella na Paul Ndunguru wakiwa wamepewa shavu.
Proud of You – Darassa na Ali Kiba wameonesha nguvu ya mapenzi kwa kusema kuwa mapenzi yanaweza kuchipua Jangwani na mapenzi hayafanyi utani na ukishikwa na mapenzi mambo lazima yatawekwa hadharani, wameonesha namna gani wanajivunia yeye (mpenzi).