Alhamisi , 11th Jun , 2015

Mume wa msani wa muziki Stecia Mayanja kutoka nchini Uganda, Abbas Mubiru amefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika biashara ya kuuza ardhi aliyokuwa anaifanya.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Stecia Mayanja akiwa na mumewe Abbas Mubiru

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, kati ya mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana huko Kampala, Mshtakiwa alichukua pesa kutoka kwa Ronald Ddanze kwa makubaliano kuwa anamuuzia kipande cha ardhi kilichopo huko Lubowa katika kata ya Wakiso.

Kesi hiyo bado inaendelea kusikilizwa na mpaka sasa, hakuna maelezo yoyote kutoka kwa msanii Stecia Mayanja kwa mashabiki wake kuhusiana na kile anachokabiliana nacho mumewe.