Picha ya Rihanna, ASAP Rocky na watoto wao wawili wa kiume
Rihanna anasema mpenzi wake na mzazi mwenziye ASAP Rocky ni baba wa tofauti, mvumilivu, kiongozi, mwenye upendo na watoto wake wanavutiwa naye.
“Nilimpenda tofauti kama baba. Ni kiongozi mkubwa, mvumilivu, mwenye upendo na watoto wangu wanavutiwa naye. Wanampenda baba yao kwa njia tofauti na ninapenda kuwaona”
“Nilikuwa natamani kuwa na watoto siku 1, kuwa sehemu ya familia, kizazi na kulea watoto zaidi ya tulivyolelewa sisi. Kitu pekee nilichofikiria labda ni paji la uso kwenye RZA ‘Komwe’ lakini Rizza Riot hana komwe”. amesema Rihanna