Jumanne , 5th Aug , 2014

Msanii wa muziki Mirror, anayefanya poa kupitia ngoma yake mpya ya Kokoro, amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa yupo mbioni kufanya project yake ya kimataifa akishirikiana na msanii Jose Chameleone.

msanii Mirror wa nchini Tanzania

Kwa mujibu wa msanii huyu, pamoja na meneja wake, Petit Man, suala hili limefanikiwa baada ya kuwa na maelewano na ukaribu mzuri na Chameleone.

Mirror ameongezea kuwa upo mpango wa kusafiri kwenda kukamilisha sehemu ya kazi iliyobakia huko Uganda muda wowote kuanzia sasa.