
Ben Pol ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba ni lazima utafute mbinu mpya za kubadilisha onyesho lako ili liwe la tofauti.
"Vile vile lazima ujifunze mbinu mpya za kubadilisha show zako, sio show iliyopita na inayokuja zifanane, hata kama unaimba nyimbo zilezile lazima utafute namna ya kuzibadilisha au kuzirearange ili zikae tofauti, au we mwenyewe presence yako au vionjo vya kwenye show yako viwe tofauti kidogo", alisema Ben Pol.
Pia Ben Pol amewashauri wasanii hao kufanya mazoezi ya kutosha, ili kuweza kujiweka sawa kimwili na mambo mengine wanapotaka kufanya onyesho.
"Naweza nikawashauri wasanii wenzangu kuboresha perfomance, kwanza mazoezi ni muhimu sana, ya viungo, kuwa na pumzi ya kutosha, kutanua kifua vizuri kwa ajili ya kuweza kuperfom kwa muda mrefu, lakini vile vile kama ni muimbaji au Rapa lazima mazoezi ya sauti pia yanamata kwa sababu huitaji sauti ikukauke au ichoke, kwa sababu unaweza ukaperfom watu wakataka urudie, au labda unaweza ukawa una set ndefu ya kuperfom, kwa hiyo mazoezi ni muhimu ya viungo na vocals pia", alisema Ben Pol.