Ijumaa , 21st Mar , 2014

Msanii wa muziki, Linex Sunday Mjeda, baada ya kusumbua sana katika chati mbalimbali za muziki na ngoma yake ya Kimugina, kwa sasa ameamua kuunganisha nguvu na Jambo Squad kutoka Arusha kupitia kolabo ambayo imesukwa chini ya studio za Noize Makers.

Linex ambaye katika rekodi za muziki wake, hii inakuwa ni kazi ya kwanza kabisa kufanya na wasanii kutoka Arusha ikiwa pia ni aina tofauti kabisa ya muziki ambayo amewahi kufanya.

Kazi hii itatoka hivi karibuni ikiwa na matarajio makubwa ya kuunganisha mashabiki wa muziki kutoka pande mbili, wale wanaokubali zaidi kazi za Jambo Squad kutoka Kaskazini mwa Tanzania, na wale wa Linex ambaye muziki wake unawavutia watu wa rika mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.