Mwanamuziki wa Injili Leah Muddy
Mwanamuziki huyo ambae awali alitokea katika mashindano ya kuibua vijana nchini amesema ameamua kuimba injili ili kuwa karibu na mungu kwa kuwa kwa sasa ameamua kubadilisha style ya Maisha yake.
Leah Muddy amesema ametumia mitindo tofauti katika album yake hiyo ambapo amesema kwa sasa yupo katika mchakato wa kukamilisha video za nyimbo zote zilizopo kwenye album hiyo kwa ajili ya kuipa nguvu zaidi na kueleweka kwa mashabiki.

