Jumanne , 9th Dec , 2014

Mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini, mzee John Kitime ameonesha sapoti yake katika wiki ya mitindo kwa mwaka huu ambapo pia mtoto wake Merlyn amekuwa ni moja kati ya wabunifu walioshiriki katika jukwaa hilo kwa mara ya kwanza na kuonesha uwezo mkubwa.

mwanamuziki mkongwe nchini John Kitime

Mzee Kitime ambaye fani yake ni Muziki, amesema kuwa amekuwa akimuona mwanae tangu akiwa mdogo akipenda kujishughulisha na mambo ya mitindo kwa njia ya michoro, blogs, mpaka sasa kushiriki katika jukwaa kubwa kama Swahili Fashion Week kupitia collection yake ya Merii Creation.