Kansiime atafanya shughuli hii sambamba na mchekeshaji mwingine mkubwa Afrika, bascketmouth kutoka nchini Nigeria ili kuongeza ladha zaidi katika sherehe hizo kwa mwaka huu.
Hii inakuwa ni nafasi nyingine kubwa kwa mchekeshaji huyo kuendelea kutangaza sanaa yake na vile vile kupeperusha bendera ya nchi yake kimataifa, kufuatia taarifa hii ambayo pia imethibitishwa na Johnson Mujungu ambaye ni meneja wake.

