Jumamosi , 19th Dec , 2015

Nyota wa muziki Cyrill Kamikaze amezungumzia kupotea kwa Wakacha muungano wa wasanii ambao kwa kiasi kikubwa uliweza kuishika tasnia ya Bongo Fleva katika kipindi cha nyuma kwa upande wa kazi nzuri za muziki na Showbiz.

Cyrill

Kwa mujibu wa Cyrill mwenyewe, Wakacha ambayo inaundwa na Cyril, Gigga Flow na Jux, pembeni ya sanaa ni familia ambayo bado ipo pamoja, umbali uliopo sasa kati yao, Jux akiwa masomoni China wakati wao wakiwa na harakati nyingine hapa bongo ukiwa ndio sababu ya kukaa muda bila kazi ya pamoja.

Nyota huyo ameahidi kurejea kwa kasi kwa kundi hilo mwanzoni mwa mwaka ujao na kazi mpya kabisa ambayo itarejesha heshima na kiki ya kundi hilo kama hapo awali.

Wakacha - Jux, Cyrill na Giga Flow