Jumatano , 29th Apr , 2015

Msanii mkongwe wa muziki hapa nchini, Hamza Kalala amezungumzia muelekeo wa muziki wa dansi hapa nchini akilinganisha na muziki wa Bongo Flava, ambapo amesema hakuna tofauti kabisa kati ya aina hizo za muziki.

mwanamuziki mkongwe nchini Hamza Kalala

Hamza Kalala ambaye ana rekodi ya kufanya kazi na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, akiwepo Lady Jay Dee, amesema hajawahi kupata tabu kufanya kazi na wasanii hawa, akiwashauri kuwekeza katika kupiga muziki wa Live na sio CD's.