Jumatano , 13th Jul , 2022

Ukiachilia mbali nafasi ya mziki kwenye maisha yake, nafasi nyingine iliyopo kwenye moyo wa msanii Jay Melody ni suala zima la mapenzi.

Picha ya Jay Melody

Hitmaker huyo wa ngoma ya Huba Hulu na Sugar amefunguka kuwa mapenzi yanachukua nafasi kubwa sana kwake na hajawahi kufikiria yanaweza kumbadilisha.

Kwa ufupi tu Jay Melody akiyaelezea mapenzi ameandika kwamba "Binafsi mapenzi yamechukua nafasi kubwa sana kwangu, sikuwahi kufikiria kama nitaweza kubadilika namna hii na yote hayo ni mapenzi".