Jumatano , 24th Jun , 2015

Star wa muziki wa nchini Kenya, Jaguar ameonesha nia ya dhati kumsaidia kijana aliyekamatwa kwa kosa la kuruka ukuta wa ikulu nchini humo, kwa lengo la kwenda kuonana na Rais Uhuru Kenyatta kumuomba fedha za kuingia studio kurekodi ngoma zake.

Jaguar

Jaguar ameeleza kuwa, amevutiwa sana na moyo wa kijana huyo aliyefahamika kwa jina Mathew Mahina akiamini kuwa hatua hiyo hatari na iliyohitaji ujasiri mkubwa aliyochukua kutimiza ndoto yake imetokana na kutoona nafasi nyingine yoyote ya kufikia mafanikio yake.

Kwa mujibu wa taarifa, kijana huyo baada ya kukamatwa alifikishwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya akili yake huku Jaguar akiwinda namna ya kuwasiliana naye ili amtimizie ndoto yake.