Jumatatu , 22nd Dec , 2014

Staa wa michano hapa Bongo, Izzo Business amesema kuwa kwa mabadiliko makubwa yaliyopo katika soko la muziki kwa sasa, inawalazimu wasanii kuwa na kitu kipya kila wakati kwa ajili ya mashabiki wao.

Rapa Izzo Bizness

Izzo ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika chati ya ngoma yake ya Mr Christmas kuwakilisha msimu huu wa sikukuu, amesema kuwa kwa sasa kuna ushindani na pia mkanganyiko katika mfumo wa kuachia kazi na vilevile kufikiri juu ya vitu vya kugusia katika ngoma, hali inayosababishwa wasanii kutokujiamini na kukariri gemu.