Isha Mashauzi
Akizungumza na eNEWZ, Isha Mashauzi amesema kwamba hakuna msanii wa taarab anayeweza kushindana nae kwa sababu nyimbo anazozitunga yeye huwa ni nyimbo zinazomhusu mama yake.
"Tangu nimeanza kufanya muziki wa taarabu sijawahi kukaa chini nikasema natunga nyimbo kwa ajili ya mtu fulani na hii inatokana na nyimbo zote ninazotunga huwa zinamhusu mama na ninafanya hivyo kwa sababu nampenda sana mama yangu na siwezi hata siku moja katika maisha yangu ya sanaa nikakaa na kuanza kutunga nyimbo kwa ajili ya kubishana na mtu", amesema.
Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa watu wanaomsema vibaya baada ya kuvaa suruali kwenye nyimbo yake na kusema kuwa anawaaribu wasanii wa taarabu hiyo sio kweli kwa kuwa yeye ni msanii na msanii ni lazima ubadilike kuendana na soko la muziki anaoufanya.
Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.