
Pichani ni Msanii Diamond Platnumz
Taarifa hii imetolewa na msanii Diamond katika insta story yake ambapo amepost mkataba ukionesha kusaini kwa msanii mpya katika label hiyo ambaye huenda akatambulishwa siku za hivi karibuni ikiwa tu ni wiki kadhaa zimepita tangu msanii Mbosso kutangaza kutoka katika label ya Wcb Wasafi
Utakumbuka ni wiki kadhaa zimepita tangu msanii Diamond kuweka wazi kutafuta wasanii watano wapya ambao atawasaini katika label hiyo na huenda huyo akawa ni mmoja kati ya wale watano aliyowaongelea msanii huyo.