Jumatano , 19th Mar , 2025

Barcelona wamepanga kuweka dau kubwa la kutaka kumnunua tena Lionel Messi kabla ya msimu wa 2026/27, kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Argentina.

 

Lionel Messi

Messi alihudumu Barcelona kwa zaidi ya miongo miwili huko Catalonia kuanzia mwaka 2000 mpaka msimu wa joto wa 2021, akijiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa huru baada ya miamba hao wa Uhispania kukosa njia ya sahihi ya kumpatia mkataba mpya.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d'Or ametumia mwaka mmoja na nusu akiwa na Inter Miami kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), huku kukiwa na tetesi kwamba Messi anaweza kurejea Barcelona, ​​​​kulingana na TNT Sports Argentina.

 

Miamba hao wa Kikatalani wanasemekana kuwa na mpango wa kumsajili nyota huyo kwa mkataba ambao utakuwa na "idadi kubwa ya masharti" mara baada ya Kombe la Dunia 2026 akiwa na umri wa miaka 39.